Mgawanyiko wa kanda za hali ya hewa Tanzania kwa ajili ya kupanda miti ya aina mbalimbali
| Kanda za hali ya hewa | Maelezo | Mifano |
| 1.Maeneo ya miinuko yenye unyevunyevu (wet montane) | Safu za milima Zaidi ya mita 1,200 juu ya usawa wa bahari na mwanzo wa ukanda wa theluji,ambapo kuna mvua nyingi isiyopungua milimita 1000 kwa mwaka. Kiwango cha chini cha joto ni 13°C.Kuna ukungu wa mawingu mara kwa mara | Lushoto,Magamba,Narok, Bunduki,Ngorongoro, Mufindi,Tukuyu n.k |
| 2.Maeneo ya Miinuko yenye Ukame (Dry Montane) |
Maeneo ya milima kati ya mita 1200 na usawa wa bahari na mwanzo wa ukanda wa theluji ambapo kwa kawaida mvua si chini milimita 760 kwa mwaka.Kiwango cha chini cha joto ni 13°C |
Shume, Njombe,Iringa, West Kilimanjaro, Meru Kaskazini, Hanang n.k |
| 3.Maeneo ya Miinuko ya Wastani (Traditional montane) |
Maeneo ya Milima kati ya mita 1,500 juu ya usawa wa bahari yenye mvua kati ya milimita 760 na 1,400 kwa mwaka. Kiwango cha chini cha joto ni 13°C | Sungwi,Olmotonyi, Rongai,Mbulu, Mbeya,Soni n.k |
| 4.Nyanda za juu zenye unyevunyevu (Moist plateau) |
Maeneo kati ya mita 600 na mita 1,200 juu ya usawa wa bahari yenyeny mvua kati ya milimita 760 na 1,400 kwa mwaka.Kiwango cha chini cha joto ni 13°C |
Geita,Manda, Tabora,Kigoma, Moshi n.k |
| 5.Maeneo yenye hali ya Ukame(Dry plateau) | Maeneo kati ya mita 600 na 1,200 yenye mvua chini milimita 760 kwa mwaka.Kiwango cha chini cha joto ni 13°C | Dodoma,Itigi, Shinyanga,Mwanza, Tabora n.k |
| 6.Maeneo ya hali ya joto na unyevunyevu(wet tropical) | Maeneo maalum katika mwambao wa pwani chini ya milima yenye mvua nyingi, na maeneo ya tambarare yaliyoko mashariki mwa baadhi ya milima.Mvua milimita 1,140 au Zaidi kwa mwaka.Kiwango cha chini cha joto ni 18°C | Rau,Kyela,Turiani, Gonja maore, Matombo,Minziro, Ukerewe,Krogwe, Muheza n.k |
| 7.Mwambao wa Pwani (Coasta belt) |
Ukanda wa Pwani chini ya mita 600 juu ya usawa wa bahari.Sehemu zingine huingia bara hadi kilomita 300.Mvua kwa kawaida ni milimita 1,000 kwa mwaka.Kiwango cha chini cha joto ni 18°C | Dar es salaam,Kibaha, Bagamoyo,Lindi, Mtwara,Ifakara n.k |
English